Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Updated at 21 Sep 2017 05:28

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Viambaupishi

  1. Mchele (Basmati) - 3 vikombe
  2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
  3. Kuku Kidari - 1 LB (ratili)
  4. Mayai - 2 mayai
  5. Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo
  6. Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
  7. Paprika - 1 kijiko cha chai
  8. Chumvi - Kiasi
  9. Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
  10. Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
  11. Tangawizi - 1 kijiko cha chai
  12. Kidonge cha supu - 1
  13. Soy sauce - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.

Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)

Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.

Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali

Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.

Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi

Wacha uchemke asilimia 70%

Chuja maji na weka kando

Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu

Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)

Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga

Kisha tia wali changanye vizuri

Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive

Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai;

.