Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Updated at 15 Feb 2017 19:02

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids. Uchunguzi unaonesha kuwa kati ya asilimia 30 mpaka 70 ya wanawake wapo kwenye hatari ya kupata tatizohili au wengine Tayari wameshalipata. Mpaka hivi sasa hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo inaelezwa kama chanzo cha tatizo hili.

JE NI NANI YUPO HATARINI ZAIDI KULIPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI?

Ni Wanawake ambao wanakaribia kukoma hedhi (Menopause) hasa wa kati ya miaka ya 38-45.
Pia Wanawake wanene au wenye Matumbo makubwa (Obesity)
Pia wanawake wasiokuwa na watoto wapo kwenye hatari zaidi ukifananisha na wale wenye Watoto.

DALILI ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI ZIPI

Tatizo hili linaweza kuwa na Dalili au Kutokuwa na Dalili kabisa. Lakini kwa mara nyingi Dalili zake ni hizi…

👉🏿Kutoka kwa Hedhi nzito pia kwa muda zaidi ya kawaida.
👉🏿Damu kutoka kipindi ambacho sio cha siku zake.
👉🏿Maumivu ya Sehemu za Kiuno.
👉🏿Maumivu ya Chini ya Mgongo.
👉🏿Kwenda haja ndogo mara nyingikwa hali isiyo ya kawaida.
👉🏿Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Sio lazima uwe na Dalili zote na mara nyingi hazitokei zote hasa ni moja au mbili.

Hivyo Kujikinga au kuepukana na Tatizo hili ni vyema kwa Mwanamke ukapungua Uzito hasa Kitambi au Tumbo kubwa.

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke;

.