Mapishi ya Biriani Nyepesi Kupika Ya Samaki

Updated at 21 Sep 2017 07:45

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mapishi ya Biriani Nyepesi Kupika Ya Samaki

Vipimo

Mchele wa pishori (basmati) - 4

Vitunguu katakata - 3

Nyanya (tungule) katakata vipande vikubwa - 3 -5

Pilipili boga la kijani (capsicum) katakata

Supu ya kitoweo au vidonge vya supu - 1

Bizari mchanganyiko Garama masala - 5-7

Pilipili mbichi ya kusaga - Kiasi

Zaafarani ya maji (flavor) - 1 kijiko cha chakula

Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe

Samaki wa kukaanga

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Roweka mchele kiasi nusu saa kisha chemsha mchele kwa supu uive nusu kiini. Mwaga maji chuja.
Wakati mchele unapikika, weka mafuta katika sufuria kubwa ya kupikia wali, kaanga vitunguu mpaka vigeuke rangi ya hudhurungi.
Tia nyanya na vitu vinginevyo vyote kaanga kidogo tu.
Mwaga wali katika sufuria na nyunyizia zaafarani kisha changanya na masala vizuri.
Funika upike katika oven (bake) au juu ya stovu moto mdogo mdogo kiasi dakika 15- 20.
Epua ikiwa tayari, pakua kwenye sahani kisha tolea kwa samaki wa kukaanga.

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mapishi ya Biriani Nyepesi Kupika Ya Samaki
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Biriani Nyepesi Kupika Ya Samaki;

.