Mapishi ya Boga La Nazi

Updated at 21 Sep 2017 07:40

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mapishi ya Boga La Nazi

Vipimo

Boga la kiasi - nusu yake

Tui zito la nazi 1 ½ gilasi

Sukari ½ kikombe

Hiliki ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi.
Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi.
Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika.
Epua mimina katika chombo likiwa tayari.

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mapishi ya Boga La Nazi
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Boga La Nazi;

.