Mapishi ya Chicken Satay

Updated at 21 Sep 2017 10:22

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mapishi ya Chicken Satay

Mahitaji

Kidali cha kuku 1 (chicken breast)
Kitunguu maji 1/2 (onion)
Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai
Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai
Curry powder 1/4 kijiko cha chai
Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder)
Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
Soy sauce 1kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai.
Chumvi kiasi (salt)
Vijiti vya mishkaki

Matayarisho

Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote (kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicken satay yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mapishi ya Chicken Satay
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Chicken Satay;

.