Mapishi ya Kidheri - Makande

Updated at 21 Sep 2017 06:26

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mapishi ya Kidheri - Makande

Mahitaji

Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo

Maharage - 3 vikombe

Mahindi - 2 vikombe

Kitunguu - 1

Nyanya - 2

Kabichi lililokatwa - 2 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai

Vidonge vya supu - 2

Chumvi - kiasi

Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula

Namna Yakutayarisha

Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi.
Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi.
Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi.
Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi.
Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive.
Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea
Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mapishi ya Kidheri - Makande
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Kidheri - Makande;

.