Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Updated at 21 Sep 2017 07:04

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Vipimo

Mchele 3 vikombe

Mboga mchanganyiko 1 kikombe

Samaki wa Pink Salmon 5 -6 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga ½ kijiko cha chai

Ndimu zilokamuliwa 2

Parsley kavu (aina ya kotmiri) 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha supu

Kidonge cha supu (stock) 2

Mafuta ¼ kikombe

Maji ½ kikombe

Namna ya Kutayarisha Na Kupika

Samaki:

Katika kibakuli kidogo, changanya; kitunguu thomu, tangawizi, chumvi, pilipili zote za unga, ndimu, parsely, bizari ya mchuzi na mafuta vijiko viwili vya supu.

Pakaza kwenye samaki.

Weka vipande vya samaki katika treya ya oveni kisha uchome (grill) huku ukigeuza hadi samaki awive. Epua weka kando.

Wali:

Osha mchele roweka kisha uchemshe uive nusu kiini

Mwaga maji uchuje mchele

Weka mafuta katika sufura, tia mboga mchanganyiko kakaanga kidogo

Weka vidonge vya supu, tia maji ½ kikombe, tia chumvi kiasi

Mimina mchele uchanganye vizuri, kisha funika hadi uive wali ukiwa tayari

Pakua katika sahani pamoja na samaki

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon;

.