Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

Updated at 21 Sep 2017 07:48

Edited By, Melkisedeck Shine, at 2017.



Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

Vipimo

Mchele basmati, pishori - 3 vikombe

Vitunguu katakata - 2

Nyanya/tungule katakata - 5 takriban

Viazi/mbatata menya katakata - 3 kiasi

Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia

Hiliki ya unga - ½ kijiko cha chai

Kidonge cha supu - 2

Chumvi - kisia

Mafuta - ½ kikombe

Maji ya moto au supu - 5 takriban

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha na roweka mchele
Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange.
Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo.
Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana.
Tia mchele ukaange chini ya dakika moja.
Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo.
Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau.
Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile

[MUHIMU HII] Msimu huu usipitwe na dawa hii muhimu ya kuandalia shamba

Soma na kutoa Maoni kuhusu Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mapishi ya Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga;

.